Washington Post imeandika kuwa: Vita vya kibiashara vya Trump vimesababisha matatizo yasio na kifani katika mfumo wa biashara, ambayo matokeo yake yameathiri uchumi wa dunia na kusababisha hasara kubwa ambayo haikutabiriwa.
Kwa mujibu wa gazeti hilo la Marekani, ushuru wa tarakimu tatu wa Trump dhidi ya China na hatua za kukabiliana na Beijing zinatarajiwa kupunguza biashara kati ya mataifa hayo mawili yenye uchumi mkubwa duniani kutoka kilele chake cha hivi karibuni cha karibu dola bilioni 700 kwa mwaka hadi karibu sufuri.
Ikulu ya Rais wa Marekani ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba bidhaa zinazoingizwa Marekani kutoka China sasa zitatozwa ushuru wa kwa uchache asilimia 145.
Mbali na kujibu mapigo kwa hatua hizo za serikali ya Trump, serikali ya Beijing imeyaweka makampuni sita ya Kimarekani katika orodha ya mashirika yasiyoaminiwa na wakati huo huo imezidisha jitihada za kidiplomasia za kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN).
342/
Your Comment